Mchezo wa hisani uliofanyika Juni 15, 2024 Zanzibar, kwa ushirikiano na Samatta Foundation, AliKiba Foundation, Fei Toto & Bui Foundation, na Safe Haven Foundation, ulikuwa tukio la kipekee.
Katika kampeni hii, Shirika la Ushirikiano na Maendeleo la Uturuki (TİKA) limeweza kusaidia safari ya elimu ya watoto wenye ulemavu katika wilaya ya Kilwa. TİKA imechangia viti vya magurudumu (wheelchair) na mashine za kuchapisha maalum kwa watu wenye ulemavu wa kuona (Braille Embossing Machine) zitakazo saidia kuongeza fursa za elimu za vijana hao.
Wakati wa sherehe ya utoaji wa vifaa hivyo, Mfaume Sudi, Afisa tawala wa wilaya ya Kilwa, alisisitiza kwamba msaada wa TİKA utasaidia katika kukuza na kutoa umuhimu kwa jamii haswa katika kuwasaidia vijana wa makundi hayo maalum.
Pia Mkurugenzi wa Samatta Foundation Hasbuna Habibu alitoa shukrani kwa TİKA kwa niaba ya AliKiba, Fei Toto & Bui, na Safe Haven Foundation kwa ushirikiano wao katika kampeni ya Nifuate Zanzibar 2024.
Mkurgenzi wa TİKA Tanzania Filiz Şahinci alisisitiza kuwa kuwezesha kuwasadia wanafunzi wenye ulemavu kuutabadilisha jamii na kuweza kuwarahisishia kuendelea na masomo yao. Hatua hii ya maana imletea mwangaza mpya wa matumaini katika safari za elimu za watoto wenye ulemavu Kilwa.