Kundi la Hamas limesema kuwa wapatanishi wa mzozo kati ya Israel na kundi hilo bado hawajatoa taarifa zozote kuhusu mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza.
Katika taarifa yake, Hamas pia imeishutumu Israel kwa mkwamo uliopo, ili kupata wakati na kuzuia duru ya sasa ya mazungumzo, kama ilivyofanya katika duru zilizopita.
Hamas imetoa matamshi hayo wakati wapatanishi wa Qatar na Misri, wakiungwa mkono na Marekani, wakiongeza juhudi wiki hii ili kukamilisha makubaliano ya kusitisha mapigano yenye lengo la kumaliza vita vya miezi tisa huko Gaza.
Pia kwa lengo la kuwaachilia huru mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas na Wapalestina wengi waliofungwa jela nchini Israel.