Serikali wilayani Chato Mkoani Geita inatarajia kuanza ujenzi wa Jengo kubwa la Upasuwaji wa Moyo na MIshipa ya Damu ifikapo 2025 Katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato ambapo huduma zote za Upasuaji kwa sasa Zinatolewa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato Bi. Husna Abdallah katika Maandalizi ya Kuwapokea Madaktari Bingwa na Bobezi wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu katika Hospitali hiyo kuanzia Julai 15 na 17 Mwaka.
Aidha Bi. Husna amesema huduma hizo zitahusisha uchunguzi wa Huduma za Matibabu ya Magonjwa ya Presha , Sukari , Magonjwa ya Moyo pamoja na mishipa ya Damu huku wataalamu wakitumia nafasi hiyo kuwapa elimu ya Tiba lishe Bora ambayo itawasaidia wananchi wa kanda hiyo kuepukana na magonjwa hayo.
Amesema lengo la uwanzishwaji huduma hizi katika Hospitali ni kuwanusuru wananchi wa kanda ya ziwa ikiwemo Geita , Kagera , Mara ,Shinyanga , Simiyu na Mikoa ya Jirani pamoja na chi za Jirani kama Burundi , Rwanda na Uganda kutolana na Vifo vinavyosababishwa na Magonjwa hayo kukithiri.
Ameendelea kustma Zaidi ya wananchi 3400 tayari walikwisha kutibiwa na kupimwa na kati yao wananchi 576 waligundulika kuwa na Matatizo ya Presha , Sukari na Magonjwa ya Moyo ambapo walipatiwa matibabu na wengine kutibiwa huku wakiwa chini ya Uwangalizi wa Madaktari.