Manchester United wamemfanya mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Joshua Zirkzee kuwa usajili wao wa kwanza msimu wa joto na enzi ya Ineos – kwa ada ya €42.5m (£35.8m) kutoka Bologna.
Mshambulizi huyo amekubali mkataba wa miaka mitano Old Trafford, na chaguo la msimu zaidi.
Zirkzee, ambaye aliiwakilisha nchi yake kwenye michuano ya Euro, alianza soka lake la kulipwa katika klabu ya Bayern Munich kabla ya kuhamia Italia kabisa mnamo 2022 baada ya kucheza kwa mkopo Parma na Anderlecht.
Msimu uliopita alishinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa Serie A chini ya miaka 23, akimaliza kama mfungaji bora wa Bologna walipofuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
United walikuwa na hamu ya kusajili mshambuliaji baada ya kufunga mara 58 pekee msimu uliopita wakiwa njiani kumaliza nafasi ya nane.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa na kipengele cha kuachiliwa kwa €40m lakini United ililipa pesa za ziada ili kuwaruhusu kueneza ada hiyo kwa miaka mitatu.