Rais Joe Biden ametoa wito kwa Marekani hivi punde siku ya Jumapili jioni Julai 14 kwa umoja, siku moja baada ya jaribio la mauaji dhidi ya rais wa zamani wa Marekani, ambaye alijjeruhiwa kidogo sikioni.
Biden alianza hotuba yake kwa kuwaambia “Wamarekani wenzake” juu ya “haja ya kutuliza joto la siasa zetu”.
“Milio ya risasi jana kwenye mkutano wa hadhara wa Donald Trump huko Pennsylvania inatutaka sote kurudi nyuma,” alisema.
Joe Biden na Donald Trump wote wametoa wito siku ya Jumapili jioni kwa Wamarekani kuwa kitu kimoja, siku moja baada ya jaribio la mauaji ya rais wa zamani kutoka chama cha Republican.
“Lazima tuje pamoja kama taifa,” rais wa Marekani alisema kwa ufupi katika Ikulu ya White House, akisema alikuwa na “mazungumzo mafupi, lakini mazuri” na Donald Trump Jumamosi jioni. Joe Biden alisema aliamuru “uchunguzi huru” kuhusu mazingira ya jaribio la mauaji dhidi ya Donald Trump.