CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam kwa kushirikiana Chuo kikuu Cha Zhejiang kutoka China wamefungua Mkutano wa Pili unawakutanisha wataalamu wa elimu kada ya sayansi kwa lengo la kuwasaidia wataalamu hao kutambua namna bora ya ufundishaji wa masomo ya sayansi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu,Prof .Peter Msoffe wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa UDSM Jijini Dar es Salaam.
Aidha Prof. Msoffe ameeleza kuwa nchi ipo katika maboresho makubwa ya mtaala wa elimu ambao unasisitiza elimu ya sayansi, suala la Hisabati, utafiti pamoja na ubunifu.
“Ukiangalia kwa makini mtaala wetu mpya unamtaka Mwanafunzi au yule anaejifunza aweze kupambana na yyanayotokea sasa au yaale yajayo,maana yake ni kwamba tunamtengeneza tunamtengeneza Mwanafunzi atakayetumika hapa Tanzania aau katika dunia”ameeleza.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye amesema kuwa mkutano huo umefanyika kutokana na matokeo ya tafiti zilizofanywa ambapo watafiti nchini watapata wasaa wa kueleza matokeo ya tafiti zao jinsi zinavyoweza kuisaidia jamii.
Naye Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu Cha Zhejiang amesema urafiki kati ya China na Tanzania unatoa nafasi ya kubadilishana walimu wa masomo ya sayansi ambapo yataleta tija kwa maendeleo ya dijitali na kuchagiza ongezeko la wasomi wa kidijitali.