Good news ninayotaka kukupatia ni kwamba Kampuni ya GSM Tanzania imeamua kushirikiana na kipindi cha Zogo Mchongo kinachomilikiwa na CRDB Bank.
Akizungumza Mkurugenzi, GSM Tanzania, Yassir Nassor amesema…‘Sisi kama GSM Tanzania tumeamua kushirikiana na CRDB baada ya kufuatilia zogo Mchongo msimu wa kwanza, na tumeona kwamba ni platform nzuri kwaajili ya kuwasaidia watanzania kutatua matatizo yao na kujipatia fursa kupitia Zogo Mchongo’ – Mkurugenzi, GSM Tanzania Yassir Nassor
Show hii kali ya Zogo msimu wa pili itarushwa kila siku Jumanne kupitia Clouds TV saa tatu usiku na marudio yake yatarushwa Jumatano saa nane Mchana na Jumamosi saa nane mchana lakini pia Show hii inapatikana kwenye Youtube platfrom ya CRDB’- Mkurugenzi, GSM Tanzania Yassir Nassor