Waziri Mkuu wa Japani Fumio Kishida ameomba radhi siku ya Jumatano kwa waathiriwa wa sheria ya ukandamizaji ambayo imepitwa na wakati ambayo ilisababisha kulazimishwa kufunga kizazi kwa maelfu ya watu katika visiwa vya Japani kati ya mwaka 1948 na 1996.
Takriban watu 16,500 walifungwa kizazi kwa lazima chini ya sheria. Mahakama Kuu ya Japani iliamua mapema mwezi Julai kwamba sheria hii ilikuwa kinyume na katiba, na kwamba muda wa ukomo wa miaka 20 haungeweza kutumika kwa madai ya fidia ya waathiriwa, ushindi mkubwa kwao.
“Wajibu wa serikali katika kutekeleza sheria hii ya kufunga kizazi ni nzito mno,” Bw. Kishida almesema mjini Tokyo. “Ninaomba msamaha wa dhati kwa niaba ya serikali,” amesema, akiinamia kundi la waathiriwa. Fidia nyingine ya kifedha italipwa.
Pia ameahidi kuchukua hatua zaidi ili kuhakikisha kuwa waathiriwa wanapokea fidia pamoja na malipo ya yen milioni 3.2 (karibu euro 18,500 kwa bei ya sasa) iliyotangazwa mnamo mwaka 2019, ambayo ilionekana kuwa dhaifu sana.
Serikali, ambayo iliomba msamaha mnamo mwaka 2019, inakubali kwamba karibu watu 16,500 walilazimishwa kufunga kizazi chini ya sheria. Kulingana na mamlaka ya Japani, watu zaidi ya 8,500 walifungiwa kizazi kwa idhini yao, ingawa wanasheria wanasema pengine “walilazimishwa” kufanya hivyo kutokana na shinikizo.