Rais wa Marekani Joe Biden amesema anajisikia vizuri baada ya kupimwa na kupatikana na maabukizo ya viruso vya Corona wakati wa safari ya kampeni yake huko Nevada siku ya Jumatano.
“Ninajisikia vizuri,” amesema mgombea huyo urais wa chama cha Democrat mwenye umri wa miaka 81 alipokuwa akipanda ndege ya rais “Air Force One.”
Tangu mdahalo wake dhidi ya Donald Trump mwishoni mwa mezi Juni, shaka kuhusu afya ya rais huyo wa Marekani, mwenye umri wa miaka 81, kumesukuma karibu wanachama zaidi ya ishirini wa chama cha Democrat kumtaka ajiondoe kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Novemba.