Marekani imetangaza vikwazo vipya vya viza dhidi ya Waisraeli ambao wamefanya vitendo vya “vurugu” dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, na kuitaka Israel kuwawajibisha watu hao.
“Hii ni kuhusu mwelekeo mpana wa kuongezeka kwa ghasia ambazo tumeziona kwa masikitiko katika miezi iliyopita na haja ya Israel kufanya zaidi kuwawajibisha watu,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Matthew Miller aliwaambia waandishi wa habari.
Hatua hizo zinawazuia Waisraeli fulani na wapendwa wao kuingia Marekani. Miller alisema serikali ya Israel imechukua “baadhi ya hatua za kukabiliana na ghasia za walowezi katika Ukingo wa Magharibi,” kama vile kuwakamata baadhi ya wahalifu.