Mtoto mkubwa wa Zlatan Ibrahimovic, Maximilian, amesaini mkataba wake wa kwanza wa kitaalamu na AC Milan.
Fowadi huyo chipukizi atachezea wachezaji wa akiba wa Milan, “Milan Futuro,” kwenye Serie C katika kampeni za 2024-25.
Maximilian, 17, alichezea kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 18 msimu uliopita. Mchezaji huyo mzaliwa wa Uswidi amemfuata babake kote Ulaya na hapo awali alisajiliwa katika akademi za Paris Saint-Germain na Manchester United.
Zlatan, ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Uswidi akiwa na mabao 62 katika mechi 121, alistaafu soka msimu uliopita wa joto baada ya mkataba wake na AC Milan kumalizika.