Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye (MB) amesema Serikali inatekeleza Mradi wa ujenzi wa Minara 758 unaogharimu zaidi ya Bilioni 200 utakaonufaisha wananchi Milioni 23.6 kupata huduma bora za Mawasiliano ya intaneti, data na simu.
Nape amebainisha hayo alipokua Wilayani Sengerema akiendelea na ziara ya kukagua Mnara wa mawasiliano katika Kisiwa cha Lyakanyasi huku akibainisha kuwa wilaya hiyo itanufaika kwa kujengewa minara 2 kati ya 17 inayojengwa Mwanza.
“Minara hiyo inajengwa na makampuni ya simu na inagharimu fedha nyingi ambapo zaidi ya Milioni 350 zinatumika kwa mnara mmoja kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga zaidi ya Tshs. Bilioni 2.4 kwa ajili ya kujenga minara 17 katika kata 16, vijiji 52 na inatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 296, 410 wa wilaya 5 za Magu, Ilemela, Sengerema, Misungwi na Ukerewe.