Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Anazungumza na Machifu Chamwino Ikulu Dodoma leo tarehe 20 Julai, 2024.
“Machifu waheshimiwa mna imani kubwa ya watu na jamii zinazowazunguuka. Au jamii mnazoziongoza. Mna dhamana ya sheria za kimila, ni dhamana yenu nyie. Na mnapowaita watu na mkawahukumu kwa sheria za kimila hawarudi nyuma”-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Na ndio maana ule mfano niliotoa wa yule mwanamke kuchapwa kwa sababu viongozi wa kimila pale wakiongozwa na chifu walitoa maamuzi yale. Kawekwa kwenye mti, katandikwa bakora za kweli kweli. Sasa ukija kwa upande mwingine ule ni wa amani na kukiuka haki ya yule mwanadamu, kwa hiyo hatutaki tufike huko machifu. Sitapendezwa kuona polisi wanakuja kumkamata chifu nayeheshimiwa kwenye jamii kwa kvunja sheria za aina hiyo,”Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.