Mchezaji anayelengwa na Manchester United Martin Zubimendi tayari amekataa kuondoka Real Sociedad msimu huu wa joto.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania, 25, amekuwa akihusishwa pakubwa na kuhamia Arsenal tangu mwisho wa msimu huu baada ya kufanya vizuri kwenye La Liga katika miaka michache iliyopita.
Naye Zubimendi, mzalishwaji wa akademi ya Real Sociedad, pia sasa yuko kwenye rada za United huku Mashetani Wekundu wakitaka kumleta kiungo mkabaji baada ya kuwasajili Joshua Zirkzee na Leny Yoro kutoka Bologna na Lille mtawalia.
Wakati ikiripotiwa kuwa Manuel Ugarte wa Paris Saint-Germain ndiye anayelengwa na klabu hiyo, gazeti la The Manchester Evening News limeeleza kuwa Zubimendi pia analengwa na United, ambayo ilitatizika katika Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita chini ya Erik ten Hag.