Everton wanachukua hatua zaidi huku wakitafuta kumshawishi Jarrad Branthwaite kusalia katika klabu hiyo.
Branthwaite anawindwa sana na Manchester United, ambao maombi mawili ya beki huyo yamekataliwa.
United walikuwa na ofa ya awali ya pauni milioni 35 pamoja na pauni milioni 8 kama nyongeza kwa Branthwaite iliyokataliwa. Baadaye walirudi na ofa ya pauni milioni 45 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 5, ambayo pia ilikataliwa.
Everton wamesimama kidete na thamani yao ya Pauni Milioni 70 kwa Branthwaite, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza England dhidi ya Bosnia na Herzegovina mwezi uliopita.
Branthwaite alikuwa amekubali masharti ya kibinafsi kabla ya kuhamia Old Trafford, ambayo ingemfanya apate pauni 160,000 kwa wiki.
Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror, Everton wako tayari kumpa Branthwaite kandarasi mpya yenye nono kubwa huku wakipania kumbakisha klabuni hapo. Branthwaite kwa sasa anapokea takriban £40,000-kwa-wiki lakini hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa kiasi kikubwa.
United walitumia pauni milioni 52 kumnunua beki wa kati Leny Yoro mwenye umri wa miaka 18. Aidha, kikosi cha Erik ten Hag pia kinafikiria kumnunua beki wa Bayern Munich Matthijs De Ligt. Everton wameripotiwa kuifahamisha United kwamba mbinu zaidi za kumnunua Branthwaite hazikubaliki.