MASHIRIKA ya vijana,wadau wa maendeleo na serikali leo wamekutana jijini Dar es Salaam ili kujadili namna bora ya vijana kuweza kukabiliana na mabadiliko hasa ya kiuchumi na changamoto za sheria na sera zinazohusu mashirika ya vijana .
Tangu kuingia madarakani kwa serikali ya awamu ya sita mabadiliko ya sheria yamerahisisha usajili wa mashirika mbalimbali hasa ya vijana kutokana na usajili huo kufanyika kwa njia ya mtandao.
Akizungumza wakati wa mdahalo,Ofisa ufuatiliaji na thamini mwandamizi ofisi ya msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali ,Charles Komba amesema wamejadili kuhusu changamoto na fursa kwa mashirika ya vijana na vijana kwa ujumla kutokana na ongezeko lao.
“ Tunazungumza mabadiliko mbalimbali ya sheria yaliyofanyika ,miongozo iliyoandaliwa na serikali kama sehemu ya kuimarisha mazingira wezeshi na tangu mwaka 2019 kufanya marekebisho ya sheria mtu akiingia kwenye mfumo kuna ongezeko la mashirika ya vijana kuna yanayoongozwa na vijana na yanayotoa afuza za vijana.
Aidha amesema miongoni mwa changamoto walizoainisha ni uanzishwaji wa baraza la taifa vijana ambayo inasimamiwa na kuratibiwa na ofisi ya waziri mkuu ,upatikana wa misamaha ya kodi kwa mashirika ya vijana na namna mamlaka ya mapato Tanzania wanaweza kuweka kundi maalum kwa mashirika yasiyo ya kiserikali.
“Kwa mazingira ya sasa mashirika yasiyo ya kiserikali yanawekwa kwenye kundi moja la makapuni na hivyo wanatozwa kodi kama wanatengeneza faida na TRA wamesema wanaanza kutafuta ufumbuzi,”ameeleza.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Tanzania bora Initative, Ismail Biro amesema wanaangalia ni kwa namna gani wanaweza kuleta mabadiliko ya sheria na sera yatakayostawisha uwezo wa mashirika ya vijana kuweza kutoa shughuli za kimaendeleo.
“Tulikuwa tunajiuza ni sheria na sera na mipango upi tunahitaji kujumulisha kwa pamoja ili kuweza kuwa wadau namba moja ya maendeleo nchini na kuna mabadiliko ambayo yametokea kama Covid -19 na uchumi wa dunia kushuka tunajiuliza tunawezaje kushirikiana na serikali na wadau kujenga mazingira ya vijana kusonga mbele.
Amesema lengo lingine ni kujenga umoja ,mshikamano ,maridhiano, hali ya kuamini baina ya wadau wa maendeleo ,vijana kwa vijana ,vijana na wadau pamoja na serikali.
“Tunatengeneza mashirika ambayo yanaweza kustahimili mabadiliko mbalimbali kama ya kiuchumi kwa pamoja tunaungana wote na ofisi ya msajili,TRA na wadau wa maendeleo kutoa huduma kwa vijana na kutoa huduma zaidi.
Naye Ofisa Mwandamizi idara ya maendeleo ya vijana –Ofisi ya Waziri Mkuu ,Nasibu Richard amesema mwitikio wa vijana katika fursa za kitaifa na kimataifa umekuwa mkubwa kwasababu Rais Samia amefungua mahusiano ya kidiplomasia yamezidi kuimarika na vijana kufika majukwaa ya kimataifa.
“Nimekuwa nikiratibu hilo kwa muda na ushiriki upo kwa kiasi kikubwa vijana wanasafiri kuiwakisha nchi Rais ameruhusu vijana kuonesha mahitaji hao,kupaza sauti zao na kushirki katika program mbalimbali kwa kutoa mawazo,bajeti na mipango ya serikali
Ameeleza kuwa serikali imeendelea kuhakikisha vijana wanapata mikopo kwaajili ya mitaji.
Amesema serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu imekuwa ikitoa fedha kwa vijana kuanzisha na kuendeleza biashara zao na wanaratibu maonesho ya kimataifa ambapo vijana wanajitangaza.