Watu wenye silaha waliwauwa watu 26 katika shambulizi dhidi ya kijiji kimoja katikati mwa Mali katika eneo lililokumbwa na waasi la Mopti siku ya Jumapili, afisa wa eneo hilo alisema Jumatatu.
Shambulio hilo lililenga kijiji kimoja katika Mzingo wa Bankass, moja ya maeneo kadhaa kaskazini mwa Mali na katikati mwa Mali ambapo makundi yenye silaha yanaendesha uasi mkali.
Washambuliaji waliokuwa na silaha waliwafyatulia risasi wanakijiji waliokuwa wakifanya kazi katika mashamba yao Jumapili jioni, Meya wa Bankass Moulaye Guindo alisema kupitia simu.
Wanajeshi waliotumwa katika eneo hilo walifika kijijini tu baada ya shambulio hilo, Guindo alisema, akisikitishwa na hali mbaya ya ukosefu wa usalama katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.