Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris alifungua mkutano wake wa kwanza wa kampeni tangu Rais Joe Biden atangaze kumuidhinisha yeye kuwa mgombea rais,kwa kuongoza kwa wingi wa wafuasi takribani 3000 na kwa asilimia mbili zaidi ya kura dhidi ya Donald Trump wa Republican hii ni kwa mujibu wa ripoti za situo cha habari cha Reuters.
Hali hiiyo inalinganishwa na upungufu wa pointi mbili ambao Bw. Biden alikabiliana nao dhidi ya Bw. Trump katika kura ya maoni ya wiki iliyopita kabla ya kuondoka kwenye kinyang’anyiro hicho Jumapili.
Kura hiyo mpya ya maoni iliyofanywa Jumatatu na Jumanne, ilifuatia Kongamano la Kitaifa la Republican ambapo Trump mnamo Alhamisi alikubali rasmi uteuzi huo na tangazo la Biden Jumapili kwamba anaondoka kwenye kinyang’anyiro hicho na kumuidhinisha Harris.
Mwanamama kamala Harris na Bw. Trump walikuwa wamefungana kwa asilimia 44 katika kura ya Julai 15-16, na Trump aliongoza kwa asilimia moja katika kura ya Julai 1-2, wakiwa ndani ya tofauti sawa ya makosa.
Ingawa tafiti za nchi nzima zinatoa ishara muhimu za uungaji mkono wa Marekani kwa wagombeaji wa kisiasa, mataifa machache yenye ushindani kwa kawaida huelekeza usawa katika Chuo cha Uchaguzi cha Marekani, ambacho hatimaye huamua ni nani atashinda uchaguzi wa urais.
Takriban 56% ya wapiga kura waliojiandikisha walikubaliana na taarifa kwamba Harris, “ndiye bora na mkali kiakili na anaweza kukabiliana na changamoto,” ikilinganishwa na 49% ambao walisema sawa na Trump,
Ni 22% tu ya wapiga kura walimpima Biden kwa njia hiyo.