Agosti 01,2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kusafiri kwa treni ya mwendokasi kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma safari ikiwa ni hamasa kwa wananchi kutumia usafiri huo.
Taarifa ya safari hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule wakati akizindua mpango wa bodaboda na bajaji kushirikiana na mkoa wa Dodoma ambao umeendana na maandalizi ya safari ya kwanza ya treni ya mwendokasi inayotarajiwa kuanza safari zake Julai 25,2024 kutoka Dar Es Salaam hadi Dodoma pamoja na maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika mkoa wa Dodoma.
“Kesho mtaanza kutoa huduma kule na hiyo kesho mpaka tarehe 31 biria wataendelea kuja na kuondoka lakini mheshimiwa Rais atakuja amepanda treni kutoka Dar Es Salaam mpaka Dodoma tarehe 01,08,2024 siku hiyo wote twende tukampokee kwasababu ukimpokea haurudi tupu ni utaondoka na abiria mabehewa yatakuwa yamejaa” Rosemary Senyamule mkuu wa mkoa wa Dodoma