Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi linamshikilia mtuhumiwa Marco Daud Zagamba (32) wa Mbweni Zanzibar kwa kosa la Kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo aliwatapeli wananchi watano na kujipatia fedha taslim shilingi 6,000,000 (Miioni Sita).
Mtuhumiwa huyo kwa nyakati tofauti aliwatapeli wananchi kwa kujifanya yeye ni mtumishi wa umma na kwamba atawasaidia kuwapatia ajira za Vikosi Maalum vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kwa kutumia mbinu hiyo mtuhumiwa alijipatia fedha shilingi 4,600,000/= (Milioni nne na laki sita) kutoka
kwa wananchi wanne wakazi wa Zanzibar.
Katika hatua nyingine mnamo tarehe 22/07/2024 huko Maisara Zanzibar,mtuhumiwa huyo alimtapelimwananchi fedha shilingi 1,400,000 (Milioni moja na laki nne) akidai yeye ni mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) na kwamba atamsaidia kumpatia ajira kwenye Idara hiyo huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa
Mtuhumiwa huyo amefanya matukio ya utapeli kwa muda mrefu akitumia mbinu ya kuwa karibu na ofisi za serikali ili kuwaaminisha anaowatapeli kuwa ni mtumishi wa taasisi hizo na anapofanikisha utapeli huo kutoweka.
Hivyo nitoe wito kwa wananchi katika kipindi hichi ambacho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Afande IGP.
Camillus Wambura ametangaza usaili kwa vijana walioomba ajira za Jeshi la Polisi.