Katika tukio la kutisha lililoripotiwa kutoka China, mwanamume mmoja alilazimika kuondolewa mboni ya jicho la kushoto baada ya kumuua nzi usoni.
Madaktari hawakuweza kupata tiba ya tatizo lake na hakuna dawa zilizoweza kutibu maambukizi kwa kuwa ugonjwa huo ungeweza kuwa mbaya, ilibidi madaktari watoe jicho lake.
Mwanamume huyo aliyetambuliwa na South China Morning Post kwa jina la Wu, alimuua nzi aliyekuwa akimsumbua baada ya mdudu huyo kumtambaa usoni kwa muda.
Saa moja baadaye, alianza kupata maumivu katika jicho lake la kushoto ambalo lilikuwa jekundu na kuvimba.
Alitafuta ushauri wa matibabu lakini maumivu hayakupungua na alianza kupata matatizo ya kutoona.