Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC,Imewashauri Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA,kuangalia namna ya Kupunguza Kodi ya Malighafi ya kukarabati Boti za Wavuvi Ili kuongeza ufanisi na uimara wa boti na kuongeza Mapato ya uvuvi na kunuvaisha Halmashauri ya Bagamoyo tofauti na sasa ambapo gharama kubwa kupata ghafi na zinasababisha Serikali kukosa mapato yatokanayo na Shughuli za Uvuvi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TASAC Nahoda Mussa Mandia wakati wa Ziara katika Bandari ya Bagamoyo kwa ajili ya kukagua ufanisi na miundombinu ya Bandari hiyo na kutembelea mwalo wa Kaole na Chuo cha Uvuvi Mbegani huku akiendelea kuiomba Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA kuhakikisha inaweka Miundombinu mizuri katika Bandari hiyo Ili wafanyabiashara na wasafirishaji kupitia njia ya majini waweze kushawishika kutumia Bandari hiyo.
Kwa upande wake, mwendeshaji wa boti, Bwana Mohamed Mwinyijuma alisema boti za faiba ni imara na salama ila vifaa vyake vina gharama kubwa.ameiomba Serikali kusaidia kuunguza gharama kwa kupinguza kodi ili wajenzi boti hizo watumie zaidi vifaa hivyo.
“Gharama za ujenzi wa boti za faiba (fibre materials) ziko juu tunaomba Mamlaka ya Mapato Tanzania ipunguze kodi”, amesema Bwana Mohamed Mwinyujuma.
Kwa sesa ya vyombo iliyofanyika mwaka 2022 Tanzania ina jumla ya vyombo vidogo 52,189 vinavyofanya shughuli za uvuvi na usafirishaji wa abiria na mizigo.
Ziara ya Bodi ya Wakurugenzi TASAC inaendelea na ziara mwambao mwambao mwa bahari ya Hindi.