Aliyekuwa Mwigizaji na Msanii wa Muziki wa Bongofleva, Snura Anton Mushi (@snuramushi ) ametangaza kuacha muziki rasmi na kuamua kumcha Mungu baada ya kufanya kazi hiyo kwa muda wa zaidi ya miaka kumi.
Snura ametanga uamuzi huo leo July 29,2024 lakini akiwa ameshautelekeza kwa miaka miwili mpaka sasa na kuzifuta video za nyimbo zake YouTube akisema hatamani kuona Watotoo wake wanakuja kusema kuwa Mama yao ni Msanii.
Miomgoni mwa Sababu nyingine alizozitaja Snura za kuchukua uamuzi huo ni pamoja na Mume wake ambaye alikuwa akimshauri mara kwa mara yeye kufanya maamuzi hayo.