Kundi la Hezbollah la Lebanon limelaani mauaji ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh siku ya Jumatano, na kuonya kuwa kifo chake kitaongeza tu azma ya makundi ya “upinzani” yanayoungwa mkono na Iran.
“Kuuawa shahidi kwa kiongozi Haniyeh … kutaongeza azma na ukaidi wa wapiganaji wa mujahidina katika pande zote za muqawama na kutafanya azimio lao kuwa na nguvu zaidi katika kukabiliana na adui Mzayuni,” Hezbollah ilisema katika taarifa yake.
Kundi hilo lilimuelezea Haniyeh kama “mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani wa wakati wetu ambao walisimama kishujaa dhidi ya mradi wa hegemony wa Marekani na uvamizi wa Wazayuni”.
Wakati huo huo serikali ya Taliban ya Afghanistan ilisema Jumatano mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh katika nchi jirani ya Iran ni “hasara kubwa”, ikimsifu kama “kiongozi wa Palestina mwenye akili na mbunifu”.
“Alifaulu na kuacha masomo ya upinzani, kujitolea, subira, uvumilivu, mapambano na kujitolea kivitendo kwa wafuasi wake,” msemaji wa serikali ya Taliban Zabihullah Mujahid alisema katika taarifa.