Serikali ya Korea Kaskazini huwa inasifika sana kwa usiri kuhusu mtawala wake , kutoka kwenye maisha ya kibinafsi hadi kwwenye maisha yake kisiasa , kutoka kwenye afya hadi kwenye familia na yote yanawekwa kuwa siri hadi yatakapojitokeza kuwa na changamoto na
Shirika la kijasusi la Korea Kaskazini limewajulisha wabunge maema wiki hii kwamba mamlaka ilikuwa ikitafuta dawa mpya kutoka nje ya nchi ili kumtibu Kim, ambaye anadaiwa kupambana na masuala kadhaa yanayohusiana na afya, ikiwa ni pamoja na uzito kupitiliza, shinikizo la damu pamoja na kisukari.
Kulingana na gazeti la ‘Los Angeles Times’, mtawala huyo wa Korea Kaskazini ana umri wa miaka 40 tu, ana urefu wa futi 5, inchi 8, lakini awali alikuwa na uzito wa pauni 308 na ameingia kwenye kundi lililo hatarini zaidi ya ugonjwa wa moyo.
Ingawa Kim Jong Un alipungua uzani na kuwa mwembamba mnamo 2021, kanda za hivi majuzi za vyombo vya habari zinaonyesha kuwa ameongezeka uzito tena.
Chombo hicho cha habari pia kiliripoti kuwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini anajulikana kwa unywaji pombe kupita kiasi na uvutaji sigara ,mbali na hilo, anatoka katika familia yenye historia ya matatizo ya moyo kwani baba yake na babu yake walifariki kutokana na matatizo ya moyo
Shirika kuu la kijasusi la Korea Kaskazini National Intelligence Service limewaambia wabunge hao katika mkutano wa faragha kwamba Kim Jong Un kwa mara nyingine tena ameongezeka uzito, ameonyesha dalili za unene kupitiliza, shinikizo la damu na kisukari, na dawa zitaletwa ili kumtibu.