Takriban watu 109 waliuawa wakati wa makabiliano makali ambayo yalitikisa Bangladeshi siku ya Jumatatu, siku ambayo Waziri Mkuu Sheikh Hasina alijiuzulu na kutoroka nchi, polisi na madaktari wamesema, wakirekebisha idadi ya hapo awali.
Hii ni siku mbaya zaidi tangu kuanza kwa maandamano ya kupinga upendeleo wa watu kupata ajira katika utawala mapema mwezi Julai, huku idadi ya vifo ikifikia 409, kulingana na ripoti ya shirika la habari la AFP iliyotolewa kutoka kwa data za polisi, afisa na vyanzo vya hospitali.
Makabiliano nchini Bangladeshi yaliendelea siku ya Jumatatu, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 109, kulingana na takwimu zilizopatikana kutoka kwa polisi na hospitali, zikirekebisha idadi ya hapo awali.
Maandamano haya yalisababisha Waziri Mkuu Sheikh Hasina, 76, kujiuzulu na kutumia helikopta kutoroka nchi siku ya Jumatatu. Jeshi limechukua madaraka na kutangaza kutoa nafasi kwa wadau wa kisiasa na wanaharakati wa mashirika ya kiraia kushiriki katika serikali ya mpito.