MAAMUZI yaliyochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, yameiwezesha sekta ya tumbaku nchini kukua na kufika namba mbili Afrika kwa uzalishaji wa sekta hiyo.
Wakati Rais Samia anachukua madarasa ya urais, Tanzania ilikuwa inazalisha tani 65,000 za tumbaku wakati leo nchi inazalisha tani 122,000 na kuiwezesha kushika namba mbili Afrika kwa uzalishaji nyuma ya Zimbabwe.
Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa Kiwanda Cha Sigara Cha Serengeti, kilichopo mkoani Morogoro, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema tumbaku yote itakayozalishwa na wakulima mashambani itanunuliwa.
“Sasa wakulima wataondokana na ‘grade’ ya uuzaji wa tumbaku kiwandani, maana nchi yetu sasa haitabakiza tumbaku majumbani kama zamani na kukuza uchumi wa wakulima na nchi yetu,” Alisema Dkt. Samia.