Niger imetangaza kwamba inavunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Ukraine.
Siku mbili zilizopita, ilikuwa moja ya washirika wake wa karibu, Mali, ambayo ilifanya uamuzi huo baada ya kushindwa vibaya mwishoni mwa mwezi Julai kwa jeshi lake na wanamgambo wa Wagner wa Kirusi huko Tinzaouatène, kwenye mpaka na Algeria.
Bamako inaishutumu Kyiv kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi wakati wa vita hivi.
Ni kwa mshikamano na serikali ya Mali na raia ambaoo Niger inavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine. Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya Niger siku ya Jumanne Julai 6 , Kanali-Meja Amadou Abdramane, msemaji wa serikali, anashutumu “vitendo vya uchokozi” kwa upande wa Kyiv na “uungaji mkono wa ugaidi wa kimataifa”.
Mwishoni mwa mwezi wa Julai, waasi kutoka Mfumo wa Kimkakati wa Kudumu (CSP) na wanajihadi kutoka kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (JNIM) walidai kuwauwa makumi ya wanajeshi wa Mali na wanamgambo wa Kirusi kutoka kundi la mamluki la Wagner huko Tinzaouatène, kaskazini mwa Mali. Baada ya vita hivi ambapo jeshi la Mali lilikiri kupoteza wanajeshi wengi katika safu zake, msemaji wa idara ya ujasusi ya Ukraine alithibitisha kwamba nchi yake ilitoa “taarifa muhimu ambazo ziliwezesha mafanikio ya kijeshi dhidi ya wahalifu wa vita wa Urusi”.