Kufuatia anguko kubwa la waziri mkuu, mshindi pekee wa tuzo ya Nobel wa Bangladesh Muhammad Yunus atahudumu kama mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo, taarifa rasmi ilisema.
Uamuzi huo, uliothibitishwa na katibu wa waandishi wa habari wa rais Joynal Abedin, ulifikiwa wakati wa mkutano uliohusisha Rais Mohammad Shahabuddin, wakuu wa vikosi vya jeshi la nchi hiyo na viongozi wa Harakati ya Wanafunzi wa Kupinga Ubaguzi, ambayo iliongoza kwa wiki kadhaa za maandamano ya kupinga serikali
Mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2006 Muhammad Yunus amesema yuko tayari, kuchukua nafasi ya mkuu wa serikali ya mpito nchini Bangladeshi baada ya kuvunjwa kwa Bunge.
Nimeguswa na imani ya waandamanaji wanaotaka niongoze serikali ya mpito,” Muhammad Yunus ameliambia shirika la habari la AFP. “Siku zote nimekuwa nikiweka siasa mbali lakini leo, ikiwa ni lazima kuchukua hatua nchini Bangladeshi, kwa nchi yangu, na kwa ujasiri wa watu wangu, basi nitafanya,” ameandika, huku akitoa wito wa kufanyika kwa “uchaguzi huru”.