Eliud Kipchoge, Mkenya anayetaka kuweka jina lake katika vitabu vya historia ya michezo ya kukimbia kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris, Tarehe 10 Agosti mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 39, atatafuta nafasi ya kuwa mtu wa kwanza kushinda mara matatu mfululizo katika mbio za marathoni katika michezo ya Olimpiki.
Atapambana na wakimbiaji wachanga, lakini pia atakuwa na changamoto nyingine ya kupambana na hali ya hewa. Joto katika mji mkuu wa Ufaransa ni kali, na huongezeka hadi nyuzi joto 30.
“Mashindano yatakuwa magumu sana – karibu 40% ni milima – na nadhani joto litachangia ugumu,” ameviambia vyombo vya habari.
Kutoka mwinuko wa kuanzia wa mita 36 kutoka usawa wa bahari katikati mwa jiji, njia hiyo itapanda hadi mita 183 kwenye barabara ya Versailles, kuelekea mwinuko wa pili mkali wa mita 172 kabla ya kuifikia alama ya kilomita 30 wakati wakimbiaji wanaporejea Paris. .
Mashindano yataanza saa 02:00 asubuhi kwa saa za Ufaransa, na Kipchoge amebadilisha mfumo wake wa mazoezi katika kituo chake cha Kaptagat katika jitihada za kuongeza medali nyingine ya dhahabu, mbali na zile za Rio, Brazil 2016 na Tokyo, Japan 2020.
“Nitaweka akilini mwangu kuhusu ukimbiaji wa milimani na katika joto kali ili kuufanya mwili wangu umudu kuelekea mashindano ya Paris,” alielezea katika mahojiano wakati wa maandalizi yake.
“Wakati mwingine hufanya mazoezi saa nne asubuhi, tano ili kuhisi joto hilo. Lakini katika Olimpiki hatuzingatii muda.”