Kesi inayomuhusu kiongozi wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma dhidi ya rais wa sasa Cyril Ramaphosa imeahirishwa hadi 2025.
Jacob Zuma anamshtaki mrithi wake kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya mwendesha mashtaka na mwanahabari ambaye, Zuma anadai, alifichua rekodi zake za matibabu wakati wa kesi yake ya ufisadi ya ununuzi wa silaha mnamo Septemba 2021.
Mahakama Kuu ya Gauteng Kusini mjini Johannesburg iliahirisha kesi hiyo hadi Februari 6, 2025, ili kuruhusu michakato ya rufaa katika Mahakama ya Kikatiba kukamilika, vyombo vya habari vya serikali ya Afrika Kusini vinaripoti.
Zuma anamshutumu Ramaphosa kwa kushindwa kufanyia kazi malalamiko yake dhidi ya mwendesha mashtaka John Downer na mwanahabari mkuu wa masuala ya sheria Bi Karyn Maughan, ambaye alidai kuwa alikiuka sheria za mashtaka kwa kupata rekodi zake za matibabu.
Mahakama ilisema Zuma atakapofika tena Februari mwaka ujao, atatarajiwa kuipatia mahakama maelezo kuhusu mchakato wa kukata rufaa.
“Kulingana na rasimu ya amri, ya tarehe 6 Agosti 2024, inaamriwa – baada ya kusikiliza mawakili ya mwendesha mashtaka wa kibinafsi, kesi ya jinai inaahirishwa hadi tarehe 6 Februari 2025.
Mwendesha mashtaka wa kibinafsi [Zuma] katika hatua hiyo , ithamini mahakama kuhusu maendeleo yoyote katika kesi hiyo,” Jaji Dario Dosio alitoa agizo hilo.