Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Samu Omorodion.
Uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 unadaiwa kuwa na thamani ya takriban pauni milioni 35 na ni tofauti na mkataba huo ambao unatarajiwa kumfanya Conor Gallagher kujiunga na Atletico kwa ada kama hiyo.
Chelsea wanataka kusajili mshambuliaji mpya na Omorodion ameruhusiwa kuondoka Atletico baada ya miamba hao wa Uhispania kuafikiana kwa pauni milioni 81 kumsajili Julian Alvarez kutoka Manchester City.
Omorodion, ambaye ni sehemu ya kikosi cha Uhispania ambacho kimefikia mechi ya medali ya Dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki huko Paris, alifunga mabao nane katika mechi 35 za La Liga msimu uliopita akiwa kwa mkopo Alaves.
Chelsea pia wanasalia kumtaka mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen.
Mkataba wa Omorodion umezungumzwa wakati wa mazungumzo kati ya Chelsea na Atletico kuhusu Gallagher, ambaye anatarajiwa nchini Uhispania wiki hii kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kukamilisha uhamisho wake wa Chelsea.
Atletico pia wapo kwenye mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa Valencia Javi Guerra lakini Chelsea hawatarajii mpango huo kuathiri uhamisho wowote wa Gallagher.