Naibu waziri wa elimu sayans na Teknolojia Omari kipanga mbunge wa jimbo la Mafia amesema kuwa ameridhishwa na maonesho ya nane nane Kanda ya masharki yanayofanyika katika viwanja vya nane nane Morogoro katika sekita za kilimo na uvuvi ambapo amewataka wakulima kutumiant teknolojia Ili kujikomboa kiuchumi.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mhe. naibu waziri amesema kuwa licha ya kutumia maonesho haya kama sehemu ya kutalii pia wakulima na wafugaji watumie ubunifu unaoonyeshwa katika maonyesho haya ili kuboresha kilimo kama kupata mbegu Bora ambazo zinastahili ukame
Aidha amesema kuwa maonesho haya ya nane nane yataleta chachu kwa wakulima kwani asilimia kubwa yamelenga katika ubunifu mbalimbali unaofanywa na wadau mbalimbali
Mh Naibu waziri ametembelea vibanda mbalimbali katika viwanja vya nane nane Mkoani Morogoro ikiwemo sekta za uvuvi na kilimo