Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekemea tabia ya baadhi ya vyama vya upinzani kutumia majukwaa ya kisiasa kuhubiri chuki na ubaguzi.
Ameeleza kusikitishwa na baadhi ya Wanasiasa wa vyama vya upinzani kusambaza taarifa za kibaguzi na kubeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Dk. Mwinyi ametoa tanko hilo katika Ziara ya kukutana na Kamati za Siasa za Matawi, Wadi na Majimbo ya Mikoa ya Zanzibar ambapo leo tarehe: 07 Agosti 2024 amezungumza na wajumbe wa kamati za Siasa wa Mkoa Mjini Kichama, ukumbi wa CCM Mkoa Amani.
Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020 – 2025 Dk. Mwinyi amesema Chama Cha Mapinduzi kimefanikiwa kwa asilimia 100 hivyo wanachama wana kila sababu ya kujivunia mafanikio hayo.
Kuhusiana na masuala ya Uwanja wa Ndege na Bandari Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Mwinyi amebainisha kuwa Serikali imeingia mikataba ya uendeshaji wa taasisi hizo na sio kuzibinafsisha kama inavyodaiwa na wapinzani.