Wakati vuguvugu la Endbadgovernance likitangaza maandamano mapya ya raia, kuanzia Oktoba 1, 2024, Rais Bola Ahmed Tinubu bado hajazungumzia kuhusu muda huo uliotolewa. Rais wa Nigeria amekuwa kimya tangu hotuba yake Jumapili Agosti 4. Maandamano ya kupinga utawala mbovu yalimalizika Jumamosi hii, Agosti 10, 2024 baada ya siku 10 zenye msukosuko zaidi kote nchini Nigeria.
Rais Bola Ahmed Tinubu alitangaza, wakati wa kampeni yake ya uchaguzi, kwamba ilikuwa zamu yake ya kuongoza Nigeria. Bola Ahmed Tinubu leo anakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa kisiasa katika historia ya nchi hiyo.
Kijadi kama ngome ya machafuko ya kijamii, Kusini-Magharibi mwa Yoruba maandamano yalifanyika bila vurugu nyingi au uporaji. Katika majimbo manne na haswa Lagos, Kusini Mashariki maandamano hayakuitikiwa na watu wengi. WViongozi kadhaa kutoka jamii ya Igbo walitoa wito wa kususia maandamano hayo kwa”kuhofia hali mbaya zaidi”.
Maandamano yaligeuka kuwa machafuko huko Kaskazini mwa Hausa na kati ya jamii mbalimbali ambapo magavana kadhaa walilazimika kutangaza sheria ya kutotoka nje.
Maandamano mengi ya amani yaligeuka kuwa vurugu na kuripotiwa visa vya uporaji. Kuonekana kwa bendera za Urusi, ambazo zilitolewa maoni mengi katika nyanja ya kisiasa, hazikuficha vifo vya waandamanaji kadhaa waliouawa kufuatia madai ya kupigwa risasi na polisi au jeshi. Siku hizi kumi za maandamano ni dhibitisho kwamba Nigeria iko katika hali mbaya.
Rais Tinubu atalazimika kushawishi waandaaji wa maandamano ili kuzuia nchi yake kuingia katika mzozo mkubwa kuanzia Oktoba 1, 2024.