Mwanamume mmoja huko Philadelphia nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka kadhaa baada ya kukiri kosa la kumuua bila kukusudia jirani yake kufuatia mzozo ambao mamlaka zinasema ulikuwa ni kuhusu kukoroma kwa sauti kubwa.
Christopher Casey, 56, kutoka Upper Moreland amehukumiwa wiki iliyopita katika mahakama ya Montgomery miezi 23 jela ikifuatiwa na kipindi cha majaribio cha miaka mitatu baada ya kukiri shtaka la kuua bila kukusudia na kumiliki silaha aliyoitumia katika uhalifu huo.
Casey awali alishtakiwa kwa mauaji ya kiwango cha tatu katika kifo cha Januari 14 cha Robert Wallace mwenye umri wa miaka 62, ambaye aliishi karibu na nyumba yake wakishiriki ukuta wa nyumba zao pamoja.
Wallace alipatikana umbali wa futi 50 kutoka kwa makazi hayo akiwa na jeraha la kuchomwa kisu wakati polisi walipofika, ofisi ya mwanasheria wa wilaya ya Montgomery imethibitisha.