Nchini Guinea, rasimu ya Katiba iliwekwa wazi usiku wa Jumapili Agosti 11 kuamkia Jumatatu Agosti 12 na Baraza la Kitaifa la Mpito.
Hili litamaliza kipindi cha mpito kinachoongozwa na Jenerali Mamadi Doumbouya tangu mapinduzi ya mwezi Septemba 5, 2021. Sheria mpya ya Msingi itapigiwa kura kabla ya mwisho wa mwaka, kabla ya kufanyika uchaguzi.
Inapendekeza mfumo wa pande mbili na kikomo kwa mamlaka ya rais kwa mihula miwili.
Rasimu ya Katiba iliwekwa mtandaoni jana usiku saa 6:20na kwa kiasi fulani inarudia yale yaliyotangazwa Julai 29 wakati wa uwasilishaji wake kwa waandishi wa habari. Kama jambo geni, rasimu hiyo inaanzisha, katika Ibara yake ya 41, jamhuri ya pande mbili yenye Bunge la Kitaifa na Seneti ambayo itaundwa kama taasisi mpya.
Kuhusu mahakama kuu, imebainishwa katika ibara ya 44 kwamba “muda wa mamlaka ya Rais wa Jamhuri ni miaka mitano, ambayo inaweza kurejeshwa mara moja tu”.
Kama ulinzi, imeandikwa kwamba “hakuna mtu anayeweza kuhudumu zaidi ya mihula miwili kama Rais wa Jamhuri katika maisha yake”.
Lakini bado kuna utata kuhusiaa na kesi ya Mamadi Doumbouya. Akiwa madarakani kwa takriban miaka mitatu, baada ya kumpindua rais wa zamani Alpha Condé, mkataba wa mpito unaonyesha kuwa hataweza kugombea katika chaguzi zijazo.