Wakati Zimbabwe ikichukua usukani wa uenyekiti wa SADC kuanzia tarehe 18 Agosti 2024 hadi tarehe 17 Agosti 2025, nchi hiyo iko tayari kuonyesha uwezo wake na kukaribisha ulimwengu katika ufuo wake na hii itakuwa fursa kwa vijana kuonesha uwezo wao hasa kwenye kukutana na watu mashuhuri wenye uwezo wakushiriki mipango yenye maendeleo endelevu.
Kaulimbiu ya ‘Zimbabwe Imefunguliwa kwa Biashara’ inaangazia matarajio ya taifa ya kufufua uchumi wake, kukuza utalii, maono na ndoto na kuimarisha uhusiano wa kikanda.
Nchini Tanzania na jirani (Malawi na Zambia),kutaandaliwa hafla za kitamaduni, maonyesho, au sherehe zinazosherehekea hadithi za Zimbabwe, muziki, sanaa, vyakula, Ubunifu, ndoto, miradi, talanta za kipekee na hadithi za Hai.
Hii sio tu itaonyesha utajiri wa Zimbabwe lakini pia itakuza mabadilishano ya kitamaduni na mshikamano miongoni mwa mataifa ya SADC.
“Zimbabwe, nchi iliyo katikati mwa Afrika Kusini, inatoa tajriba tele ambayo itakuacha ukiwa na furaha isiyokoma kuanzia Maporomoko ya Victoria hadi magofu ya kale ya Zimbabwe, nchi hiyo imezama katika historia, utamaduni na asili na uzuri wa kipekee.
Kupitia programu ya SADC Live Your Dream Road Tour na Moving Arts safari yakuyaona yote haya itaanzia nchini Tanzania hadi Zimbabwe kuanzia 16 October 2024 hadi 18 novemba 2024., kukuza maendeleo ya vijana, kubadilishana utamaduni, na ushirikiano wa kikanda.
#SADCLiveYourDream