Mwanadada aliyetajwa kuwa nyota wa mtandao wa kijamii wa India amekamatwa na kuzuiliwa baada ya video yake iliyoonyesha akipika na kula ndege wa taifa wanaolindwa nchini humo, tausi, polisi walisema.
Polisi walisema kwamba Kodam Pranay Kumar alizuiliwa Jumatatu na kupelekwa jela baada ya “video zingine kwenye simu yake ya mkononi kuthibitisha” kwamba ndege ambaye alikuwa amempika alikuwa tausi.
Ndege hao wa rangi mbalimbali hulindwa chini ya sheria kali za wanyamapori.
“Sasa yuko gerezani kwa siku 14 chini ya Sheria ya Ulinzi wa Wanyamapori na sasa mahakama itaamua kama angesalia ndani au kupata dhamana,” Akhil Mahajan, msimamizi wa polisi katika jimbo la kusini la Telangana aliiambia AFP.
Wachunguzi pia wanajaribu kufahamu jinsi na wapi Kumar alifanikiwa kupata tausi huyo, ambayo imeondolewa kwenye chaneli yake.
Video hiyo ilimuonyesha akipika tausi, “jambo ambalo linadaiwa kuvutahisia za watu wengi zaidi,” gazeti la The Times of India liliripoti.
“Walakini, majibu yalikuwa mbali na yale ambayo angeweza kutarajia,” iliongeza.
“Watumiaji wa mitandao ya kijamii walilaani video hiyo, wakimtuhumu Kumar kwa kuendeleza ulaji haramu wa wanyamapori na kudharau alama ya taifa”.