Wamiliki wa maduka ya maua huko Xiaohongshu, China wamepata hasara kutokana na vijana kutojitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya siku ya wapendanao nchini humo, inayofanyika kila mwaka, mwezi Julai au Agosti kupitia tamasha la Qixi lililofanyika mapema wikiendi hii, Jumamosi, Agosti 10, 2024.
Imeelezwa kuwa wateja waliokua wakinunua maua kwaajili ya wapenzi wao walikua wachache, baadhi ya maduka yamechapisha mzigo wa maua yaliyobaki bila kuuzwa, Alfred Wu, profesa msaidizi kutoka chuo kikuu cha kitaifa cha Singapore, amesema kuwa vijana wameshindwa kuudhuria kutokana na kutokua na kazi.
Hali ya kutokuwa na furaha pia inaathiri juhudi za serikali ya China inayohimiza ndoa kwa vijana kama njia ya kukabiliana na changamoto ya kupungua kwa viwango vya kuzaliwa watoto na idadi ya watu wanaozeeka, idadi ya watu inayopungua inaweza kuwa kikwazo katika ukuaji wa uchumi wa taifa hilo.
Katika nusu ya kwanza ya 2024, wanandoa milioni 3.43 tu walifunga ndoa, nusu ya idadi hiyo ilirekodiwa katika kipindi kama hicho miaka 10 iliyopita, kulingana na wizara ya masuala ya kiraia, licha ya serikali kuhamasisha watu kushiriki katika tamasha la Qixi kusherekea siku ya wapendanao vijana walionekana kuwa wachache.
Kituo cha utangazaji cha taifa hilo CCTV, kilirusha video iliyoonyesha picha za familia ya rais Xi Jinping, mkewe Peng Liyuan na mtoto wao wa kike wakisherekea ndoa yao, ambayo imedumu kwa zaidi ya miongo mitatu lakini ujumbe huo haukuweza kushawishi raia ambao wanalalamika kutoweza kuanzisha familia kwa sababu wanadaiwa pesa