Iran ilikataa mwito wa Jumanne wa nchi tatu za Ulaya ukiitaka kujiepusha na mashambulizi yoyote ya kulipiza kisasi ambayo yatazidisha mivutano ya kikanda. Iran inaita “ombi la kupita kiasi.”
Viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani katika taarifa ya pamoja Jumatatu waliitaka Iran na washirika wake kujiepusha na kulipiza kisasi mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran mwezi uliopita Iran imeilaumu Israel.
Viongozi hao wa Ulaya pia waliidhinisha msukumo wa hivi punde wa wapatanishi kutoka Qatar, Misri na Marekani kufikia makubaliano ya kumaliza vita vya Israel na Hamas.
Mazungumzo yanatarajiwa kurejelewa Alhamisi. Na walitoa wito wa kurejeshwa kwa mateka wengi wanaoshikiliwa na Hamas na utoaji “bila vikwazo” wa misaada ya kibinadamu huko Gaza.
Wapatanishi wametumia miezi kadhaa kujaribu kuzifanya pande hizo kukubaliana na mpango wa awamu tatu ambapo Hamas itawaachilia mateka waliosalia waliokamatwa katika shambulio lake la Oktoba 7 badala ya Wapalestina waliofungwa na Israel, na Israel itajiondoa kutoka Gaza.
Baada ya zaidi ya miezi 10 ya mapigano, idadi ya vifo vya Wapalestina inakaribia 40,000 huko Gaza, kulingana na Wizara ya Afya huko.