Bruno Fernandes anasema alikuwa na “ofa halisi” kutoka kwa vilabu vingine kabla ya kuamua kuongeza mkataba wake Manchester United.
Fernandes ameongeza mkataba wa mwaka mmoja, ambao utamweka Old Trafford hadi 2027, na chaguo la mwaka mwingine.
Lakini kiungo huyo wa kati wa Ureno amefichua kwamba, kabla ya kufanya uamuzi wa kusalia, kulikuwa na uwezekano wa kuondoka klabuni hapo majira ya joto.
“Kura hii ya imani kutoka kwa klabu ilikuwa muhimu sana kwangu,” Fernandes alimwambia Thiago D’Amaral wa ESPN Brasil.
“Hata kwa sababu nilifuatwa [na vilabu vingine], klabu ilijua kwamba kulikuwa na uwezekano wa mimi kuondoka, nilikuwa na ofa thabiti.
“Lakini klabu ilionyesha kwamba ilinihitaji, kwamba ilikuwa wakati wa mabadiliko na kwamba walitaka kufanya mambo tofauti.”