Mkuu wa mkoa Morogoro Adam Malima amewataka watendaji wa Kata kuacha kufanya upendeleo wakati wa kushugulikia Changamoto za ardhi katika maeneo yao
Rc Malima ameyasema hayo wakati akifungua semia Kwa watendaji wa kata na maafisa tarafa zote wa mkoa huo ambapo amesema wapi baadhi Yao wanatumia vibaya Kwa kufanya upendeleo Kwa wafugaji wakati wa utoaji mamauzi .
Anasema migogoro mingi ya ardhi inayohusisha wakulima na wafugaji inachangiwa na utendaji mbaya wa ngazi za cbini pamoja na viongozi kutumia vibaya madaraka Yao.
“nimeenda Kwenye Kata Moja mkulima amelishishiwa nyanya zake mtendaji anasema alipwe Elfu 80 huku mkulima anasema amelishiwa Mazao yenye Thamani ya laki nane hii sio sawa”
Aidha Rc Malima amesema maafisa tarafa na watendaji kuhakikisha wanafatilia miradi yote ya serikali inayotekelezwa Katika maeneo Yao Ili itekelezwe kwa ubora unaotakiwa.
Anasema ni lazima ufuatiliaji ufanyike kuanzia ngazi ya vijijini hadi mkoa kila.mradi Ili Thamani ya miradi iendane na ubora wa miradi .
RC Malima awataka Maafisa Tarafa, watendaji wa Kata kuwajibika.
Pia amesema moja ya changamoto inayowakabili maafisa hao ni kutokuwa na ubunifu katika utendaji kazi wao hivyo amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa kata wawe wabunifu ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo wanayosimamia.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Simoni maganga amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maafisa Tarafa na Watemdaji wa Kata ili kuweza kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yalianza Juni 6, 2023 katika Mikoa ya Songwe, Njombe, Katavi na Rukwa na kubakiza Mikoa nane ambayo yatafanyika kwa mwaka wa fedha 2024/ 2025.