Katika kuhakikisha Chama cha Ushirika wa kuweka na kukopa cha Jeshi la Polisi Tanzania usalama wa raia Saccos Urasaccos umeendelea na ziara za kimafunzo ndani na nje ya nchini ambapo leo Agosti 15,2024 wamefika katika kiwanda cha uzalishaji wa nguo cha A to Z kilichopo Jijini Arusha nakuona namna ambavyo wenzao wanavyoendesha Saccos zao.
Wajumbe wa Urassacos wakiongozwa na mwenyekiti wa bodi hiyo kamishna wa Polisi CP Suzan Kaganda wamesema wamejifunza namna bora ya kuendesha Saccos ambapo wamepata elimu yanmna ya kukua kiuchumi na kuweka vitega uchumi ambavyo vitaendelea kuboresha mapato ya saccos yao.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo CP Kaganda ameongeza kuwa mafunzo waliyoyapata katika kiwanda hicho yamewafungua kifikra ambapo ameahidi kwenda kuka na wajumbe wa bodi kutekeleza mipango na mafunzo mazuri waliyoyapata.
Anna Hashimu ambaye ni Mwenyekiti A to Z Saccos licha ya kuwapongeza mambo mazuri yanayofanya na usalama wa raia Saccos ameahidi kuweka mpango mkakati wa mashirikiano baina ya URASACOS na ATOZ Saccos ili kuboresha huduma kwa wateja wa saccos hiyo.