Vyombo vya habari mbalimbali vimesema kuwa vimepata takwimu za hivi punde kutoka kwa wizara ya afya ya Gaza kuhusu idadi ya wahanga katika eneo hilo tangu shambulio la Hamas la Oktoba 7 dhidi ya Israeli.
Wizara hiyo inasema Wapalestina 40,005 wamefariki katika mashambulizi yaliyofuata ya Israel.
Watu wengine 92,401 wamejeruhiwa, mamlaka iliongeza.
Takwimu hizi hazitofautishi kati ya raia na wapiganaji.
Kwingineko mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza yanaendelea huko Doha, kulingana na ripoti.
Mazungumzo hayo magumu yanalenga kujaribu kuwatoa mateka kutoka Gaza na kurejesha usitishaji mapigano.
Idadi ya waendeshaji wa kimataifa wanashiriki katika mazungumzo hayo lakini sio Hamas kwa sasa.
Mkuu wa kijasusi wa Israel anatarajiwa kuungana na mawaziri wenzake wa Marekani na Misri na waziri mkuu wa Qatar kwa ajili ya duru mpya ya mazungumzo.