Shirika la afya duniani, WHO, limetangza ugonjwa wa MPOX kuwa janga la dharura la kimataifa la afya, kwa mara ya pili kwa kipindi cha miaka 2, hasa baada ya mlipuko wa ugonjwa huo katika taifa la DRC na ambao umesambaa kwa mataifa jirani, kama vile Burundi, Uganda na Kenya.
Haya yanajiri wakati huu nchi ya DRC ikiwa ndio imeathirika zaidi na maambukizo ya Mpox, kituo kinachotoa huduma kwa wagonjwa mjini Bukavu kikiendelea kuwahudumia wagonjwa.
Hospitali hii ya chuo kikuu cha Bukavu imetoa nafasi kutoa huduma kwa wagonjwa wa Monkey Pox. Iragi ni miongoni, aliyefika kupewa matibabu na baadaye kurudi nyumbani.
‘‘Ona jinsi mwili wangu ulivyo. Hapa nawashwa zaidi! Hasa ninapopewa dawa. ilianza polepole kama vile upele kwenye sehemu ya siri, na sasa imeenea mwili mzima.’’ Alisema Iragi, mmoja wa wagonjwa wa Mpox.
Daktari Freddy Siangoli anahusika na uchunguzi wa magonjwa haya akiwa pia msimamizi wa huduma za matibabu ya Monkey Pox Kivu kusini, anaelezea takwimu.
“Tumepata zaidi ya wagonjwa 4000 na zaidi ya wagonjwa 25 wamafariki kutokana na Monkey Pox Kivu kusini. Ili kujikinga inabidi tuheshimu kanuni na desturi za afya zile zile kama wakati wa Uviko 19.” Alisema DaktariDaktari Freddy Siangoli.
Hata hivyo, bado shughuli zinaendelea kama kawaida Kivu kusini, wala hakuna anayejali. Hawa ni miongoni mwa wakazi wa Bukavu.