Meneja wa Liverpool Arne Slot anasema klabu hiyo bado inatafuta kuimarisha kikosi kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Wekundu hao walijaribu kumsajili Martin Zubimendi kutoka Real Sociedad lakini wakakosa nafasi baada ya kiungo huyo wa Uhispania kuamua kupinga uhamisho huo.
Inamaanisha kuwa Liverpool ndio timu pekee ya Ligi ya Premia ambayo haijafanya usajili mkubwa msimu huu wa joto, huku dirisha la uhamisho likifungwa saa 23:00 BST Ijumaa, 30 Agosti.
“Nimeshasema mara nyingi kwamba kikosi chetu kiko imara kweli na si rahisi sana kupata wachezaji ambao wanaweza kutusaidia au hata kuimarisha kikosi,” alisema Slot.
“Zubimendi alikuwa mmoja wao kuwa mwadilifu, lakini aliamua kutokuja. Tunasonga mbele na wale tulionao. [Wataru] Endo alifanya vizuri kwenye pre-season hivyo tuko mahali pazuri.
“Huku nyuma, [mkurugenzi wa michezo] Richard [Hughes] anajaribu kuimarisha kikosi awezavyo lakini, kwa bahati mbaya, Zubimendi aliamua kutokuja.
“Alifanya kila juhudi kumleta lakini, ikiwa mchezaji ataamua kutokuja, basi ni dhahiri kwamba haji.”