Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Volker Turk alilaani ghasia zinazoendelea Israel katika Ukanda wa Gaza unaokumbwa na vita, akifichua kuwa karibu watu 130 wamekufa kila siku tangu Oktoba 7.
“Kwa wastani, takriban watu 130 wameuawa kila siku huko Gaza katika kipindi cha miezi 10 iliyopita. Kiwango cha uharibifu wa jeshi la Israel wa nyumba, hospitali, shule na maeneo ya ibada kinashangaza sana,” Turk alisema.
Turk alisisitiza kuwa “hali isiyofikirika” katika eneo lililozingirwa inatokana na kushindwa mara kwa mara kwa jeshi la Israel kufuata sheria za vita.
Hayo yakijiri zaidi ya wakazi 100 haramu wa Israel walishambulia mji wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, na kuua mtu mmoja na kuchoma moto nyumba na magari kadhaa, kulingana na vyanzo vingi.