Ufilipino imegundua kisa kipya cha virusi vya homa ya nyani nchini humo cha kwanza tangu Disemba mwaka jana, Wizara yake ya afya imesema Jumatatu, na kuongeza kuwa inasubiri majibu ya vipimo kabla ya kuweza kubaini aina yake.
Mgonjwa huyo alikuwa mwanaume Mfilipino mwenye umri wa miaka 33 ambaye hakuwa na historia ya kusafiri nje ya Ufilipino, Wizara ya Afya imesema.
“Tunangoja matokeo ya vipimo na tutatoa taarifa mara tu yatakapopatikana,” msemaji wake Albert Domingo alisema alipoulizwa kuhusu matatizo hayo.
Shirika la Afya Ulimwenguni WHO Jumatano lilitangaza h oma ya nyanikuwa hali ya dharura ya afya ya umma dunian , ikiwa ni tahadhari ya juu zaidi ya shirika hilo , kufuatia mlipuko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao ulikuwa umeenea katika nchi jirani.
Aina mpya ya virusi imezua wasiwasi kimataifa kwani inaonekana kuenea kwa urahisi kwa mawasiliano ya karibu ya kawaida.