Mkurugenzi wa michezo wa Napoli Giovanni Manna anasema kuondoka kwa Victor Osimhen kwa sasa “kumezuiwa”.
Chelsea imekuwa ikihusishwa na mshambuliaji huyo majira yote ya kiangazi, huku Romelu Lukaku akipigiwa upatu kuelekea upande tofauti.
Osimhen hata amewasilisha ombi la kuhama kulazimisha kuondoka, na kocha mkuu Antonio Conte alimfukuza mchezaji huyo wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Nyote mnajua kabisa hali ya Osimhen ilikuwa tayari nilipofika na itashughulikiwa na klabu pekee,” alisema.
“Sikuingia katika hali hiyo. Nyote mnajua kuwa soko la uhamisho ni gumu sana na [mpango] kwa sasa umezuiwa. Siwezi kusema zaidi ya hilo.”
Manna amesisitiza uamuzi wa Conte, akiiambia Sky Sports Italia Jumapili: “Ni ukweli halisi, kile ambacho kocha alisema, hali imezuiwa.